Sunday 22 December 2013

ANG'ATWA SIKIO NA HAWARA WA MUMEWE KISA WIVU WA MAPENZI




Mwenyezi mungu alieumba aridhi na mbingu alimtofautisha mwanadamu na wanya mnyama amepewa akili tuu bali mwanadamu amepewa akili na utashi .Ila kwa hali ya sasa yale wanayofanya wanadamu ni kama wanatumia akili tu bila utashi unyama matukio ya ajabu kimekuwa kitu cha kawaida sana kwa dunia ya leo
Matukio ambayo zamani tulikuwa tukiyaona katika filamu ila kwa sasa yanatokea katika jamii tulizopo inasikitisha na inahuzunisha sana kuona mwanadamu mwenzio anapata maumivu yaliyosababishwa na mwanadamu mwenzie
Hivi karibuni hapa jiji mwanza mkazi mmoja wa Igoma Aliefahamika kwa jina moja la Consolata amepigwa na mmewe na kung’atwa sikio na mtu anaedaiwa kuwa ni hawara wa mumewe  bi consolata amesema alikuwa akigombana na mumewe ndipo hawara yake huyu alipokuja na musema ngoja tukuonyeshe maana hutujui ndipo alipong’atwa sikio na kuondolewa sikio zima
Mara baada ya kufanyiwa ukatili huo alienda kulipoti katika kituo cha polisi lakini kwa madai yake kuwa watuhumiwa waliachiwa kwakuwa walikuwa wakijuana na baadhi ya askari waliokuwepo kituoni .Ndipo bi consolata alipochukua hatua za kutafuta wasamalia wema kama waandishi ili waweze kumsaidia aweze kupatiwa matibabu kwani ni mgeni jiji mwanza toka kigoma na alikuja mwanza kwa ajili ya kumsalimu mumewe 
Baada ya kuzungumza na waandishi alipelekwa kwenye taasisi ya kivulini ambao mpaka sasa wanampatia huduma ya matibabu ukatili huu kiukweli ni aibu kubwa kwa taifa letu
                  









No comments:

Post a Comment