Tuesday 17 December 2013

KUMBE SIKU HIZI WASICHANA/MWANAUME BIKIRA SIO DEAL KABISA!

Leo wakati nakuja hapa nilipo muda huu nilikuwa nimeongozana na wadada kama
wa-4 hivi inaonekana wanaishi jirani na wanakofanyia kazi au wanakoishi ni kumoja.
Wadada hawa walikua na story iliyovuta masikio yangu na kunifanya nipunguze spidi ili niendelee kuwasikiliza kwa kuwa tulipokuwa pana ka umbali kidogo hadi ufikie kituo cha

usafiri wetu wa umma[Hiace/daladala/vifordi]
Wadada hawa walikuwa wanamzungumzia mwenzao ambae inaonekana siku za
karibuni ataolewa. Tatizo hapa halikuwa kuolewa bali anaemuoa.
Inasemekana kuwa huyo mume mtarajiwa wa rafiki wa hao akina dada hajawahi kufanya ngono,yaani ni bikra wa kiume.

Wadada wale walikuwa wanamlaumu mwenzao kwa kutokusikiliza maelekezo
yao kwa
kukataa kuolewa na huyo jamaa kwakuwa ni "mshamba" yaani hayajui
mapenzi kitendo kitakachomfanya rafiki yao aanze kutembeza shule kwa huyo mume namna ya kugegeda kitendo ambacho wale wadada hawakukubaliana nacho. Walionekana kukerwa sana na
walikuwa wanasema wao hawawezi kuja kuolewa au kuwa na mahusiano na mwanaume
wa aina hiyo.

Story hiyo ikanikumbusha miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nazungumza na jamaa zangu
kuhusiana na suala hili ambapo kuna jamaa alikuja kutulalamikia kuhusiana na mkewe
kutokujua mapenzi kwa sababu alimkuta bikra.

Jamaa yetu yule alionekana kukereka sana na alifikia kusema kama angejua asingemuoa. Kati ya vijana tuliokuwa pale watatu walikubaliana na yule jamaa.
Nilishangaa!Nilidhani kuwa kama ukimkuta mwanamke sio used basi unafurahi kumbe
sio.
Sasa nikiunganisha na hili tukio la leo naona hili jambo kama linakua flani hivi,yaani huenda hili suala hapo siku za nyuma lilikuwepo lakini inaonekana linachukua kasi mbaya.
Nimeamua kulileta hapa ili nijue Wanaume wa hapa wanalichukuliaje suala hili. Pia
wanawake nao wanalichukuliaje hili.
Yaani kama kuna watu wawili ambao unatakiwa uchague kati ya huyo mmoja awe
mwenzi wako na mmoja ni used na mwingine sio,ungependa yupi awe mwenzi wako na kwanini?

Watu wa siku hizi inaonekana hawapendi masuala ya kuanza kufundishana,wanataka watu ambao ni waalimu tayari.Inaonekana sisi mabikra tutaipata mwaka huu....lol!
Naomba mchango wako tafadhali! -Mdau

No comments:

Post a Comment