Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’.
MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi jijini Dar es Salaam
(GRC), Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amekiri kuwa aliwahi kukamatwa
kwa wizi wa pesa.
Mtumishi huyo wa Mungu ambaye hujiita Super Charge, alisema aliwahi
kujikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kichapo cha kufa mtu
kutoka kwa baba yake mzazi Mzee Anthony (sasa marehemu) baada ya kudakwa
na wizi wa shilingi 900 akiwa nyumbani kwao Mbeya.
Tukio hilo lilimtokea akiwa kijana ambapo kisa hicho kilimsukuma kumrudia Bwana na kuamua kumshinda shetani
Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni
kanisani kwake Ubungo- Kibangu, Dar, Mzee wa Upako alisema hawezi
kuisahau siku hiyo ambayo shetani aliamua kukunjua kucha zake kumwelekea
yeye.
“Niliwahi kuiba shilingi 900, miaka ya zamani kidogo (hakutaja) tukio
hilo lilinikumba lakini baba yangu alinipa kichapo cha kufa mtu hali
ambayo ilinipelekea kuamua kumrudia Mungu aliye hai.
“Siku hiyo nilikuwa katika mihangaiko ya maisha lakini nilijua fedha
hizo zingenisaidia kwa kipindi hicho, siwezi kusahau tukio hili maana
baba yangu alinipiga sana, ilikuwa fedheha kwangu,” alisema Mzee wa
Upako
Akizungumzia mchezo mzima ulivyokuwa, Mzee wa Upako alisema siku ya
tukio, akiwa nyumbani kwao na ndugu zake, ghafla alikuta pesa ziko
mezani kwenye chumba cha baba yake, aliamua kuzikwapua, lakini siku
iliyofuata alitokea baba yake na kumshushia kichapo cha viboko ambavyo
idadi yake haikumbuki.
“Hakika zilikuwa ni siku za majaribu kwangu, kukamatwa kwa tuhuma za
kujihusisha na wizi wa pesa lilikuwa ni jambo ambalo sijawahi kulifanya
achilia mbali kuliwaza kabisa, lakini siku hiyo sijui ilitokea nini
nikajikuta nimenasa mtego huo mbaya na mchafu dhidi yangu,” alisema.
Licha ya kukaa kwa miaka kadhaa, njia sahihi ilikuwa ni kumrudia
Muumba wangu. Jambo hilo halikumfurahisha marehemu baba yangu,
alinimsamehe na kumuacha aendelee kumtumikia Mungu katika ngazi ya
uchungaji.
No comments:
Post a Comment