Thursday 26 December 2013

MWILI WA MAREHEMU WAKUTWA NA PIPI 17 TUMBONI ZA MADAWA YA KULEVYA NI BAADA YA KUPASULIWA MOROGORO.



MWILI wa marehemu, Khalid Abdul Kitala (47) ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo
jijini Dar es Salaam ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro muda mfupi kabla ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na kete 17 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya katika tukio la kufasarisha maiti iliyotiliwa shaka na askari polisi Mikumi ambao waliweka mtego kufuatia kupata taarifa za tukio hilo na raia wema na kulinasa gari lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam majira ya saa 21:26: HRS jana usiku.
Katika gari la watuhumiwa lilipekuliwa kwa kina na kupatikana kete 7 na kete 17 na kufanya jumla yake kuwa 24 zilizokamatwa na watuhumiwa wapo chini ya ulinzi katika kituo kikuu cha polisi kwa uchunguzi.


No comments:

Post a Comment